Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Kujifunza Kuhusu Agora

 

Hatua ya kwanza ni muhimu sana, haswa kama unaongoza klabu ya kwanza kwenye mji wako na hauna miundo ya kuangalia. Tunapendekeza ufuate msururu wa hatua hizi: 

1. Jiunge na Jukwaa la Agora la Mtandaoni. Huu ni mfumo wa kujiunga mara moja ambao utakupa ufikivu wa seti za huduma na mifumo amabzo zinaongezeka mara kwa mara. (Baada ya kujiunga, utarudishwa kwenye ukurasa huu).

2. Angalia uwasilishi mfupi wa utambulisho huu. dk 15

3. Sikiliza kipindi cha mafunzo kilichorekodiwa hiki. Masaa mawili

4. Soma Mwongozo wa Agora mpya siku 1-2. Jifahamishe na Wiki, haswa kwenye vipengele vifuatavyo ambavyo vinabadilika mara kwa mara na ambavyo maelezo yanaweza yakapitwa na wakati kwenye mwongozo.

5. Angalia sampuli ya mkutano uliorekodiwa (masaa mawili). Hii ni video ambayo haijahaririwa ambayo inaonyesha sehemu kubwa ya mwongozo. Imerekodiwa kwa maksudi kwa njia isiyo ya kitaalam, kuonyesha mkutano wa ukweli unavyokuwa (wenye juu na chini), badala ya kujaribu kuonyesha mkutano wa aina fulani uliopigwa video kutumia waigizaji wenye uzoefu.

6. Angalia video za mafunzo kwenye Channeli ya YouTube yetu ambazo zinaelezea na kutoa vidokezo vya majukumu tofauti. Kwenye channeli, unaweza pia ukaangalia video nyingine za mikutano iliyorekodiwa na klabu duniani kote - zote za kuwepo mahali na za mitandaoni.

Kama una mashaka yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia info@agoraspeakers.org au kwenye mitandao yetu yoyote ya kijamii (kwa mfano, kundi letu la Facebook https://www.facebook.com/groups/agoraspeakers/ ).

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:36 CEST by agora.